Home BURUDANI DK. SERERA AHIMIZA MFUKO WA SANAA NA UTAMADUNI KUJENGA UWEZO KWA WASANII

DK. SERERA AHIMIZA MFUKO WA SANAA NA UTAMADUNI KUJENGA UWEZO KWA WASANII

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Suleiman Serera ametoa wito kwa watendaji wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa (TACAF) kuendelea kuwajengea uwezo Wasanii ili waweze kunufaika na mfuko huo sambamba na kurejesha fedha walizokopa

Dk. Serera ametoa wito huo Aprili 23, 2024 Jijini Dar es Salaam alipotembelea mfuko huo kwa lengo la kujifunza shughuli zinazofanywa na Mfuko huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara.

“Amehimiza mfuko huu uendelee kutoa mikopo kwa kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa ili mikopo hii ilete tija kwa wadau husika,” amesema.

Aidha ameagiza mfuko huo kufuatilia ajira zilizotokana na mikopo iliyotolewa kwa wasanii walionufaika

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here