Home KITAIFA TFS WAKABIDHI MIZINGA YA NYUKI YA KISASA 300 RUFIJI

TFS WAKABIDHI MIZINGA YA NYUKI YA KISASA 300 RUFIJI

Na Mwandishi wetu, Rufiji

WAKALA wa misitu Tanzania (TFS) wa Wilaya ya Rufiji wamekabidhi mizinga ya nyuki ya kisasa 300 kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ), Mohamed Mchengerwa kwaajili ya vikundi vya vijana 38 vilivyoomba msaada wa mizinga hiyo.

Alikabidhi mizinga hiyo Aprili 22, 2024 Ikwiriri Wilayani Rufiji mkoani Pwani Meneja wa TFS Wilaya ya Rufiji Francis Kiondo amesema mizinga hiyo itawasaidia vijana kujiimarisha kiuchumi.

Kiondo amesema mizinga hiyo ameikabidhi kwa niaba ya Kamishina Muhifadhi TFS, Profesa Do santos Silayo amekabidhi mizinga hiyo 300 kwa Mbunge wa jimbo hilo la Rufiji iliakakabidhi kwa vikundi hivyo 38 vya vijana ambapo jumla ya vikundi 38 vilipeleka maombi ya kuomba kupewa mizinga hiyo.

“Vikundi vitatu vinakabidhiwa kwaniaba ya vikundi vingine ambapo kila kikundi kitapata mizinga ya nyuki ya kisasa kumi ambayo inauwezo wa kutoa hadi asali kilo 20 kwa mwaka ikiwa ni katika kuwasaidia uchumi wananchi wa jimbo hilo la Rufiji,”amesema.

Ametaja vikundi vitatu vilivyokabidhiwa mizinga hiyo kwa uwakilishi kuwa ni pamoja na Chama Cha ushirika wa vijana wajasiriamali, Ikwiriri shotern karate na kikundi cha UVCCM kwa Mpalange.

Akipokea Mizinga hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ameshukuru Wizara ya Maliasili na TFS kwa mizinga hiyo kwaajili ya vikundi vya vijana wa jimbo hilo na kwa ushirikiano mkubwa aliopata kutoka kwa TFS katika kipindi hiki cha mafuriko ya Mto Rufiji wilayani humo ikiwa ni pamoja na Msaada wa Boti, vyakula na maturibai.

Amesema pamoja na athari mbalimbali za mafuriko zilitokea wilayani humo lakini wamekuwa wakipata neema ya kupata mizinga hiyo ya nyuki ya kisasa kwaajili ya vikundi 38 vya vijana.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mahusiano mazuri na Wadau mbalimbali ambapo mahusiano hayo yamefanya Watu mbalimbali na Wadau wengi wa Maendeleo kuleta misaada mbalimbali ya hali na Mali kwa waathirika hao wa mafuriko ya Mto Rufiji kwa Wilaya za Kibiti na Rufiji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here