Home KITAIFA MZEE MALECELA NI HAZINA YA MAARIFA NA UZALENDO-DK.MWINYI

MZEE MALECELA NI HAZINA YA MAARIFA NA UZALENDO-DK.MWINYI

Na Mwandishi wetu, Dodoma

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Viongozi na Watanzania wanajifunza mengi kutokana na historia ya utendaji kazi wa Mzee John Malecela katika nyadhifa mbalimbali alizoshika Serikalini na Chama cha Mapinduzi na ataendelea kuwa hazina muhimu ya maarifa na uzalendo hapa nchini.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika sherehe za Kumbukizi ya miaka 90 ya kuzaliwa Mzee John Malecela, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika nyumbani kwake Uzunguni Jijini DodomaAprili, 21 2024.

“Nampongeza Mzee Malecela kwa kutimiza umri huu na amemuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia umri mrefu na afya njema,” amesema Dk.Mwinyi.

Ameeleza kuwa Watanzania wataendelea kufaidika na busara, hekima, na ushauri wake katika kuiletea maendeleo nchi yetu na uzoefu wake mkubwa alionao Mzee Malecela katika uongozi, siasa na diplomasia ya Kimataifa.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha
Mapinduzi na Dini Wamehudhuria akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Comrade Abdulrahman Kinana, Spika wa Bunge Mstaafu, Job Ndugai, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here