Home KITAIFA DK NCHIMBI ALAKIWA KWA SHANGWE NA MKUTANO MKUBWA UBARUKU, MBARALI

DK NCHIMBI ALAKIWA KWA SHANGWE NA MKUTANO MKUBWA UBARUKU, MBARALI

Na Mwandishi wetu, Mbeya

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na nderemo na wananchi wa Mbarali, wakiongozwa na vijana waendesha bodaboda, baada ya kuwasili na msafara wake katika Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, leo Aprili,18 2024, akitokea Mbeya Mjini.

Dk Nchimbi alisimama kuwasalimia wananchi hao wa Ubaruku, akiwa njiani kuelekea Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo ameambatana na Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC – Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here