Na Mwandishi wetu, ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zinafanya jitihada kubwa kukabiliana na vitendo vya rushwa na kur3yuejyhimiza uwajibikaji ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 pamoja na mipango mingine,, ya maendeleo.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua rasmi Mkutano wa mafunzo kwa wajumbe na wataalam wa kamati ya SADCOPAC katika kupambana na rushwa , kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa maliasili unaofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar leo Aprili, 162024.
Ameeleza kuwa Zanzibar inasimamia masharti na maelekezo ya miongozo ya kamati ya SADCOPAC kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatekeleza kikamilifu makubaliano yaliyoafikiwa baina ya nchi wanachama.
“Zanzibar imeanzisha utaratibu wa kusomwa hadharani taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kujadiliwa kwa uwazi na kina katika Baraza la Wawakilishi,”amesema Dk.Mwinyi.
Ametoa wito kwa nchi wanachama wa SADC kuziimarisha taasisi zinazohusika na utawala bora kwa kuzipatia wataalam zaidi wa fani mbalimbali ili ziwe na upeo mkubwa zaidi wa kufanya uchunguzi kwa mujibu wa majukumu yao.