Home KITAIFA MAJALIWA AWASILI MKOANI MOROGORO. KUKAGUA ATHARI ZILIZOSABABISHWA NA MAFURIKO.

MAJALIWA AWASILI MKOANI MOROGORO. KUKAGUA ATHARI ZILIZOSABABISHWA NA MAFURIKO.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 16, 2024 amewasili Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro ambapo atakagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi.

Pia Majaliwa atazungumza na wananchi waliothirika na mafuriko hayo.

Aidha,Majaliwa pia ataelekea Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani ambapo pia atakagua athari za mafuriko pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo ya Muhoro na Chimbi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here