Home KITAIFA RC KUNENGE APOKEA TANI 300 ZA CHAKULA KUTOKA KWA RAIS DK. SAMIA...

RC KUNENGE APOKEA TANI 300 ZA CHAKULA KUTOKA KWA RAIS DK. SAMIA YEYE BINAFSI KWAAJILI YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

MKUU wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amepokea msaada wa mchele, Maharage na unga tani 300 kutoka kwa Rais Dk. Suluhu Hassan yeye binafsi kwaajili ya waathirika wa mafuriko yanayoendelea katika Mto Rufiji kwa Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani msaada uliowakirishwa na Innocent Mbilinyi.

Akizungumza leo Aprili, 15 2024 na Waandishi wa Habari mjIkwiriri Wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati wa kupokea msaada huo Kunenge ameshukuru kwa misaada huo ambapo tayari tani 32 za mchele zimekwisha wasili na kupokelewa wilayani humo huku tani zingine zikiwa barabarani kuletwa wilayani humo.

Amesema Rais amekuwa akiwapelekea misaada mingi ya aina mbalimbali kwaajili ya Wananchi wa mkoa huo wanapopatwa na maafa mbalimbali kutoka serikalini lakini msaada huu wa tani 300 ni msaada alioutoa yeye binafsi.

” Rais amekuwa akituletea misaada mingi kutoka serikalini lakini msaada huu ametoa yeye binafsi na sisi tunaahidi tutaigawa misaada hii kwa kusimamia vizuri kwa walengwa kama ambavyo yeye imempendeza kutoa msaada huu.

“Lakini nimshukuru Mbunge wa jimbo la Rufiji na Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kwa Kazi kubwa anayoifanya ya kututafutia misaada mbalimbali na sisi tumuahidi kwamba misaada yote inayokuja tutaisimamia vizuri kwa kutumiwa na walengwa kama ilivyokusudiwa,” amesema Kunenge.

Naye Innocent Mbilinyi alikabidhi msaada huo kwaniaba ya Rais Dk. Samia Msaada huo wa mchele daraja la kwanza tani 100, maharage tani 100 na unga tani 100 ambapo tani zilizofika tayari ni tani 32 wakati tani zingine zikiendelea kuja.

Na baada ya kukabidhiwa alikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele kwaajili ya usambazaji kwa walengwa waathirika wa mafuriko katika Wilaya za Kibiti na Rufiji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here