Home KITAIFA RC CHALAMILA UHARIBIFU WA BARABARA KUTOKANA NA MVUA SERIKALI HAIJALALA IKO IMARA.

RC CHALAMILA UHARIBIFU WA BARABARA KUTOKANA NA MVUA SERIKALI HAIJALALA IKO IMARA.

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila Amewatoa hofu wananchi Dar es Salaam ametoa taarifa kwa umma kuhusu ujenzi wa barabara lukuki unaoendelea katika mkoa huo.

Akizungumza leo April 15,2024 na waandishi wa Habari Ofisini kwake Ilala Boma Chalamila amesema mvua nyingi zinazoendelea kunyesha Katika maeneo mbalimbali ya Mkoa ambayo imepelekea uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, serikali haijalala iko imara hivi karibuni miundombinu hiyo itarekebishwa na kujengwa barabara kwa kiwango cha lami.

“Mkoa huu kila wilaya barabara zitajengwa ikiwemo Ilala Kilometa 55.27, Ubungo Kilometa 54.27, Kigamboni Kilometa 42.11, Temeke Kilometa 52.71, na Kinondoni Kilometa 48.33 ambapo ametoa rai kwa wakandarasi wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi nzuri waombe kazi hiyo mara tu itakapo tangazwa, “amesema Chalamila.

Aidha amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anadhamira ya dhati katika kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi katika nyanja anuai, hivyo amewaomba wananchi kuwa watulivu kutokana na kadhia wanayoipata ambayo imesababishwa na uhalibifu wa barabara katika maeneo yao kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here