Home MICHEZO DK. NDUGULILE ATOA MAAGIZO KWA AFISA MICHEZO KIGAMBONI VIWANJA VYA MICHEZO VYOTE...

DK. NDUGULILE ATOA MAAGIZO KWA AFISA MICHEZO KIGAMBONI VIWANJA VYA MICHEZO VYOTE KUENDELEZWA

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

MBUNGE wa Kigamboni Dk.Faustine Ndugulile amekipongeza Chama cha Mpira wa miguu Kigamboni (KDFA) kwa kuandaa mashindano mazuri ya veterans.

Apongeza KDFA kwa kuanzisha mashindano hayo ya veteran cup ambayo leo Aprili 14 2024 yamefika tamati na mashindano yaliyojumuisha timu 11 kutoka wilaya yetu ya kigamboni kiukweli yalikuwa mazuri sana na fainali ya leo imewapatia burudani nzuri.

“Ndugu zangu niwaombe tuendelee kufanya mazoezi kwa ajili ya kufahamiana, kujenga urafiki na kuimarisha afya zetu mashindano haya yamekutanisha baadhi ya wachezaji wa zamani wa timu za Simba na Yanga,”amesema Dk.Ndugulile.

Ameleza kuwa fainali ilikutanisha Gezaulole veterans na kibada veterans, ambapo mchezo ulimalizika dakika 90 bila kufungana na Gezaulole veterans kuibuka bigwa wa mashindano kwa kushinda mikwaju ya penati 5 na 4 kwa Kibada veterans.

Aidha, Dkt Ndugulile amemwagiza mwakilishi wa Afisa utamaduni, Sanaa na michezo wa wilaya ya Kigamboni, Twidike Ntwima kuhakikisha viwanja vyote vya michezo vifuatiliwe na vitambuliwe ili vikabidhiwe Kwa timu za maeneo husika kwa matumizi, kutunza na kuendeleza ili kuepuka uvamizi wa viwanja vya michezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here