Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA NA WALINZI WA HAYATI SOKOINE.

RAIS DK.SAMIA NA WALINZI WA HAYATI SOKOINE.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na waliokuwa walinzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa Kumbukumbu ya miaka 40 tangu kifo chake, iliyofanyika Monduli mkoani Arusha Aprili, 12 2024.

Kulia ni aliyekuwa Mlinzi Mkuu Abihudi Michael Luila aliyekuwa gari ya nyuma wakati ajali inatokea na kushoto Mlinzi wa zamu Yusto Chuma ambaye alikuwa gari moja na Hayati Sokoine. Chuma wakati huo naye alijeruhiwa vibaya sana na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 14.

Hayati Sokoine alifariki dunia Aprili,12 1984 kwenye ajali ya gari iliyotokea Wami Dakawa Wilayani Mvomero mkoaniĀ Morogoro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here