Na Mwandishi wetu, Rufiji
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam, Abas Mtemvu ameongozana na viongozi wa CCM wa mkoa wa huo kukabidhi msaada wa mahitaji ya chakula na vifaa kwa Waathirika wa mafuriko katika kata 12 za wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa kukabithi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya milioni 22 kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji , Meja Edward Gowele huko katika viwanja vya shule ya msingi Umwe Ikwiriri amesema amekuja kutekeleza ahadi yake aliyotoa wiki iliyopita wakati alipokuja Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Abdulamani Kinana.
Amesema kuleta msaada huo ni kutekeleza agizo la Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM aliloagizwa siku hiyo alipofika kutembelea na kuzungumza na waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya ya Rufiji kwani baada ya ujio ule Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Dar es salaam akapokea simu za Wadau mbalimbali wakitaka kuchangia kutoa msaada huo kwa Waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya humo.
Amesema asili ya Dar es salaam ni mkoa wa Pwani na huwezi kuitoa Dar es salaam katika mkoa huo wa Pwani hivyo wamesema lazima waje kuleta msaada huo iliwashiriki kutoa walichonacho na wao kwa kuleta msaada huo kwa ndugu zao.
Mtemvu amesema aliporudi walikutana na kuunda timu yao iliyofanikisha kupatikana kwa misaada hiyo chakula na vifaa umetolewa na wanaCCM kutoka mkoa wa Dar es salaam na Wadau wake akiwemo Amo Foundation,
Awali Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Gowele amemshukuru kwa msaada huo kutoka kwa wanachama wa CCM, Wananchi na Wadau wa mkoa wa Dar es salaam na kusema zoezi la kuhamisha wananchi mashambani bado litaendelea ilikupisha mafuriko hayo.
Amesema tayari uongozi wa Wilaya umetenga viwanja zaidi ya 600 kwaajili ya wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo maeneo yao na eneo hilo ni salama halitakuja kufikiwa na mafuriko.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Rogart Mbowe amesema Mwenyekiti wa CCM huyo wa mkoa wa Dar es salaam baada ya kutoka Rufiji katika ziara ya na Kinana hakulala akawaagiza wenyeviti wa CCM Wilaya za mkoa wa Dar es salaam watafute misaada hiyo ilikuja kuleta kwa ndugu zao wa Wilaya hiyo walioathiriwa na mafuriko hayo.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya AMO foundation. Amina saidi ambaye amehusika kuchangia misaada hiyo zaidi ya tani kumi za unga wa sembe ambapo amezitaka Taasisi na mashirika yasiyoya kiserikali kupeleka misaada yao ya hali na Mali kwa waathirika hao wa mafuriko ya Wilaya ya Rufiji.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es salaam, Hadija Ally Saidi ametaka vyakula zaidi ya tani 13 walivyoleta kuwa ni mchele , maharage, unga wa sembe, makatoni ya maji ya kunywa, magodoro 100 hiyo yote ni matokeo ya siasa safi ya CCM kuanzia ngazi ya Taifa inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, CCM mkoa wa Dar es salaam na mahusiano na Wadau wake.
Kwa upande Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rufiji, Kaswakala Mbonde ameshukuru kwa msaada huo uliotolewa na CCM mkoa wa Dar es salaam na kuelezea kuwa hali ya mafuriko wilayani humo yanahistoria ya zaidi ya miaka 50 hivyo amewataka Watanzania kutokubali kupotoshwa kuhusu wanasema mafuriko hayo ni athari za Bwawa la kuzalisha Umeme Mwalimu Julias Nyerere.