Na Mwandishi wetu, Mwanza
MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) wa CCM, Leonard Qwihaya alikuwa Mgeni Rasmi katika Fainali ya Ramadhani cup iliyo hitimishwa Aprili,7 2024 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kirumba jijini Mwanza
Fainali hiyo ilikutanisha timu mbili ambazo ni Godon Fc Vs ambapo timu hiyo imeweza kuibuka na ushindi wa goli tatu kwa sifuri huku Timu ya Godon Fc ni bingwa wa Ramadhani cup mwaka 2024.
Pia ameongozana na Viongozi Mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Kata jirani pamoja na Katibu wa Uvccm Mkoa Joshua Ramadhani na Qwihaya alitumia fursa hiyo kuwataka vijana kumuunga Mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassani Kwa Kazi nzuri anazozifanya
Qwihaya ameongoza Maandamano ya amani kutoka Ofisi za Ccm Kata ya Kirumba kuelekea uwanja wa Shule ya Msingi Kirumba