Home KITAIFA ZAIDI YA Sh1.6 BILLIONI KUKAMILISHA MIRADI SITA YA MAENDELEO WILAYANI MWANGA

ZAIDI YA Sh1.6 BILLIONI KUKAMILISHA MIRADI SITA YA MAENDELEO WILAYANI MWANGA

Ashrack Miraji,Same

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro,Abdallaah Mwaipaya amesema jumla ya miradi Sita ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 inatarajiwa kupitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ikiwemo ya barabara, vijana, elimu, maji, afya na mazingira.

Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha hayo leo Aprili, 7 2024 katika hafla ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Kwa Mkuu wa wilaya ya Moshi,Zephania Sumaye iliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi kifaru mpakani mwa Wilaya ya Mwanga na Moshi.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Godfrey Mnzava akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyange wilayani Mwanga unatarajiwa kukamilika Mei, 20 2024 na wananchi waanze kupata huduma ya Afya Kwa wakati pia kuepuka kufuata huduma za afya mbali.

Mbali na hayo yote kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa akiwa na timu yake amesema ameridhishwa na miradi yote sita ambayo Mwenge wa Uhuru umepita.

Mnzava ametaka miradi ambayo tayari imewekewa jiwe la msingi ikamilike kwa wakati na ambayo imekamilika tayari iwe chachu ya maendeleo katika wilaya ya hiyo hasa miradi ya afya na maji.

“Hivyo nitoe pongezi za dhati Kwa Mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Mkuu wa Wilaya,kuendelea kusimamia miradi hiyo ya maendeleo na kuwasaidia vijana katika nyanja tofauti za kujikwamua kiuchumi,”amesema.

Ikumbukwe Kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 inasema “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here