Home KITAIFA MIRADI NANE YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILLION 3.6 INATARAJIWA...

MIRADI NANE YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILLION 3.6 INATARAJIWA KUZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE APRIL, 8 SAME

Na Ashrack Miraji

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema jumla ya miradi nane ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3.6 inatarajiwa kupitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ikiwemo ya barabara, vijana, elimu, maji, afya pamoja na mazingira.

Akizungumza leo Aprili 6 na mwaandishi w ofisin kwake Mkuu hwa Wilaya hiyo amebainisha hayo wakati akitoa taarifa ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 ambao utapokelewa kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Njoro asubuhi ya April, 8 ukiwa unatokea na Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.

Mgeni amesema baada ya kuupokea Mwenge utakimbizwa Wilayani humo Kilometa 138.4 katika mbio hizo miradi minne itafunguliwa, mitatu itatembelewa na mmoja utawekewa jiwe la msingi ambao ni mradi wa kwanza wa barabara uliopo same mjini.

“Niwaombe wananchi wote ambao wapo Wilayani Same wahakikishe wanajitokeza kwa wingi Shule ya Msingi Njoro kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa shamla shamla, nderemo na vifijo lakini pia kujitokeza kwa wingi kwenye mkesha wake pale uwanja wa Shule ya Msingi Hedaru,”amesema Mgeni

Pia amesema kuwa maandalizi muhimu ya kuupokea Mwenge huo tayari yamekamilika ikiwemo miradi ya maendeleo itakayopitiwa lakini pia jukwaa la viongozi pamoja na la wasanii kwenye eneo la mkesha wa Mwenge ambapo imepangwa kufanyika viwanja vya Shule ya Msingi Hedaru.

Amesema baadhi ya viongozi wa dini tofauti wa Wilayani hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kuwa wananchi wanapaswa kutambua kufika kwa mwenge Wilayani ni moja ya sehemu ya maendeleo kwao kwani miradi mbali mbali ya maendeleo itafunguliwa hivyo hawanabudi kujitokeza kwa wingi kusikiliza maelekezo muhimu kutoka kwa viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa.

Kwa mwaka 2024 mbio za Mwenge wa Uhuru zimebeba kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here