Home KITAIFA ZANZIBAR KUDUMISHA USHIRIKIANO NA OMAN.

ZANZIBAR KUDUMISHA USHIRIKIANO NA OMAN.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Oman.

Rais Alhaj Dk.Mwinyi amesema hayo leo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar, Said Salim Al Sinaw iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi Aprili 4 2024.

Pia Dk. Mwinyi amesema Serikali ya Oman imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo ikiwemo ukarabati wa majengo ya kihistoria, Afya na Elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here