Home KITAIFA DERMAK KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUTOKANA NA UONGOZI WA DK.SAMIA

DERMAK KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUTOKANA NA UONGOZI WA DK.SAMIA

Na Mwandishi wetu @Lajiji Digital

Serikali ya Tanzania na Denmark zimekubaliana kushirikiana katika maeneo ya Elimu,Afya Biashara, Uwekezaji, Nishati pamoja na utunzaji wa mazingira huku Denmark ilieleza utayari wa kusitisha nia yake ya kufungua ofisi za ubalozi kufuatia tamko walilotoa mwaka 2021.

Akizungumza Leo Aprili 3 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari baada ya kukutana na Waziri wa Denmark anayeshughulikia Ushirikiano wa Maendeleo na Sera ya Hali ya Hewa, Dan Jorgensen waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema nchi hizo mbili zinashirikiana zaidi ya miaka 50 katika masuala mbalimbali ikiwemo diplomasia.

Amesema ziara ya waziri huyo kutoka Denmark ni muhimu ni ya kwanza baada ya nchi hiyo kutoa tamko la kusitisha shughuli zake nchini mwaka 2021.

“Tumekubaliana kushirikiana katika nyanja ya elimu, afya biashara pamoja na kilimo, Tanzania inaiunga mkono Denmark katika mpango wao wa kuomba uanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” amesema Makamba.

Ameeleza kuwa ikumbukwe nchi ya Denmark ilitangaza kusitisha shughuli zake nchini na kufunga ubalozi mwaka 2021 kisha baadae kutangaza bungeni kusitisha shighuli zake nchini Tanzania kutokana na sababu za kiuchumi tamko ambalo waziri huyo amelitangaza kusitisha baada ya kuridhishwa na hali ya maendelo uongozi bora na demokrasia katika taifa la Tanzania.

Makamba amesema katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendeleza ushirikiano na kufanya mambo mazuri ikiwemo kubadilishana ujuzi na uzoefu katika mambo mbalimbali.

Aidha amesema waziri huyo yupo nchi kwa ziara ya siku mbili atatembelea maeneo mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri wa Denmark Anayeshughulikia Ushirikiano wa Maendeleo na Sera ya Hali ya Hewa, Dan Jorgensen amesema nchi ya Dermak itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja za maendeleo ikiwemo katika kukabilina na mabadiliko ya Tabia nchi kutokna na matokeo yanayo jitokeza ulimwengu kote.

Amesema wamekuwa na ushirikiano mzuri kati ya nchi hizo mbili katika maeneo mbalimbali na wataendelea kushirikiana kwa malengo hivyo ni fursa kwa nchi hizo.

“Tulikuwa na mazungumzo mazuri na waziri tumekubaliana kushirikiana katika maeneo yafuatayo, elimu, afya, biashara, uwekezaji, nishati na utunzaji wa mazingira na ushirikiano huu umeimarika kutokana na uongozi mzuri wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,”amesema Jorgensen.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here