Home KITAIFA GAVANA TUTUBA AMESEMA DOLA SIO CHANGAMOTO YA TANAZANIA PEKEE NI LA DUNIA.

GAVANA TUTUBA AMESEMA DOLA SIO CHANGAMOTO YA TANAZANIA PEKEE NI LA DUNIA.

Na Mwandishi wetu @Lajiji Digital

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba amesema suala la dola sio changamoto ya Tanzania pekee ni la dunia hivyo wanaendelea kufanyia kazi suala hilo.

Pia amesema asilimia 22 ya watanzania wanatumia huduma rasmi za kibenki hivyo kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa huduma hizo.

Hayo ameyabainisha leo Aprili 2 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mashindano yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taaluma za Kibenki (TIOB ) ya wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNCC).

Amesema hivyo Dola zipo kwenye mabenki na zilizopo serikalini kulingana na mfumo wa akiba ya nchi bado wanazo.

“Ndio maana tunaendelea kulipia miradi yote ya serikali hakuna mradi ambao umewahi kukwama au kuchelewa malipo kwasababu ya changamoto ya Dola fedha zile ni za serikali kwa sababu kupapu kusapoti kwenye uchumi wafahamu kuwa ni low season,”amesema Gavana Tutuba.

Amesema vyanzo vya kuweka fedha za Dola ni kupitia shughuli mbalimbali kwa hiyo Dola zinaendelea kupatikana kwa kiwango ambacho bado ni stahimilivu ukilinganisha na mahitaji ya nchi.

Amesema ndio maana ukisoma taarifa yao ya kuishia Disemba mwaka jana nakisi ya ulali wa biashara kulinganisha kutuma na kupokea dola mwaka juzi ilikuwa dola bilioni 5.3 lakini imepungua hadi Disemba mwaka jana ilikuwa dola bilioni 2.7.

Gavana Tutuba amesema inaonyesha kwamba shughuli za watu wengi wameendelea kuongeza kutuma na kupunguza kuingiza ndio maana nafasi kuwa ndogo bado wanaendelea kusimamia.

“Tangu mwaka 1992 walivyoingia kwenye soko huria hatuweki viwango vya reja reja sokoni na soko linajiendesha hivyo inategemea kiwango cha banki na viwango vya kubadilishia fedha vipo wazi na huru kuzingatia mifumo ya soko huria,” amefafanua.

Aidha Gavana Tutuba amesema asilimia 70 ya sekta ya fedha inashikiriwa na sekta binafsi na serikali inaweka misingi mizuri ya sekta hiyo kadri ya uchumi unavyo kua na kuimarika.

“Mwaka jana tulizindua mwongozo lengo ni kuhakikisha watanzania wote wanapata elimu ya fedha kwa sababu hawana elimu ya fedha ni nyeti wajue namna ya kutunza fedha zao,”amesema

Ameongeza kuwa kutafuta namna tofauti kuhakikisha watanzania kupata elimu na kupata maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

Ganana Tutuba amesema TIOB kuleta mashindano hayo ambayo Wamezindua leo na kuandaa viongozi wa badae ambao wataleta maendeleo chanya.

Vilevile, amesema program hiyo itawatengenezea vijana uwezo wa kutosha na ujuzi hivyo wanafunzi wa elimu ya juu wajitokeze kwa wingi kushiriki ambayo itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu.

“Mashindano hayo yataendeshwa kwa mfumo wa TEHAMA ambapo watawafikia walengwa wengi natoa wito kwa taasisi zote za elimu ya juu kuhamasisha kushiriki mashindano haya na ni fursa kwa vijana,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Tusekelege Joune amesema asilimia 70 sekta ya fedha inashikiriwa na sekta biafsi ni jukumu la sekta binafsi. kusimamia kuwa ushindani.

Amesema sekta binafsi ni wafanyabiashara pia watanzania ni wengi wanahitaji huduma za kibenki wanakaribishwa kufungua mabenki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Mususa amesema mashindano hayo yanafahamika kwa jina la”TIOB SCHOLAR BANKING CHALLENGE” yenye lengo la kuelimisha vijana jinsi ya kutoa huduma za kifedha kwa kutumia mbinu bora na kuendesha taasisi kibiashara kwa misingi bora yenye maadili na umakini.

Amesema mashindano hayo yamezinduliwa leo rasmi na yameanza leo yanatarajia kuisha Julai 7 mwaka huu wanatarajia kuwa na washirika 2000 na yataendeshwa kwa mfumo wa kidijitali kupitia mfumo wa WhatsApp.

“Taasisi ya TIOB imeandaa mitaala mbalimbali ya mafunzo kwa ajili ya kuibua vipaji na taaluma kwa wingi zaidi katika sekta ya fedha pamoja na kubuni program za mafunzo ya vitendo kwa umma wa watanzania, “amesema Mususa.

Ameongeza kuwa wanafunzi kutoka taasisi za elimu ya juu wanaruhusiwa na wanakaribishwa kujiunga na shindano hilo wakati wote kuanzia leo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here