Home KITAIFA DIWANI YUSUPH AIPONGEZA PURA KWA USIMAMIZI BORA.

DIWANI YUSUPH AIPONGEZA PURA KWA USIMAMIZI BORA.

Na Mwandishi wetu,

DIWANI wa Kata ya Songo Songo mkoani Lindi, Hassan Swaleh Yusuph ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo waJuuu wa Petroli (PURA) kwa usimamizi bora wa miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) iliofanywa na kampuni zinazozalisha gesi asilia katika kisiwa cha Songo Songo.

Yusuph ametoa pongezi hizo hivi karibuni wakati akizungumza na wataalam wa PURA walioambatana na wadau wa vyombo vya habari walipofanya ziara kisiwani humo kwa lengo la kutembelea miradi hiyo ambayo inatekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Kampuni ya PanAfrika Energy Tanzania (PAET).

“PURA imefanya kazi kubwa ya kuja na miongozo ya juu ya uwajibika ya utekelezaji wa makampuni kwa jamii itakayotoa namna bora ya utekelezaji wa miradi hii jambo ambalo limekuwa chachu kwa wananchi kupata miradi wanayoitaka na inayoendana na mahitaji yao na sio miradi inayoamuliwa na kampuni za wawekezaji, “amesema Yusuph.

Kwa upande wake Mjiolojia muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Desmond Risso amesema wamefarijika na kuona juhudi zinazofanywa na wawekezaji katika eneo hilo huku akifurahishwa na namna ambavyo diwani amewataka wananchi kutumia miradi hiyo kwa namna ambayo imekusudiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here