Home KITAIFA MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA ASKOFU WA NLGCC

MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA ASKOFU WA NLGCC

Na Mwandishi wetu, Mara

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa Machi 30 2024 alimuwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Askofu wa kanisa La New Life Gospel Community Church (NLGCC ) Jimbo la Mara Kaskazini Fransisca Gachuma ambaye pia ni mwenza wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC),Christopher Gachuma.

Majaliwa amesema Dk.Rais Samia ameguswa na msiba huo na ataendelea kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa familia ya Gachuma kwa wananchi wa Tarime na Tanzania kwa ujumla.

Naye, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema Chama cha mapinduzi kitaendelea kuyachukua mafunzo ya Marehemu ili kujiimarisha zaidi na kukijenga chama hicho.

Mazishi hayo yalifanyika katika Kijiji cha Komaswa Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here