Home MICHEZO WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

Na Chedaiwe Msuya na Asia Singano, Dodoma

WIZARA ya Fedha pamoja na Taasisi zake, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango zanzibar zimeendelea kuimarisha ushirikano wake kupitia njia mbalimbali ikiwemo michezo.

Akizungumza katika Bonanza la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Kilimani jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Lusius Mwenda, amesema michezo hiyo ni moja kati ya njia moja wapo ya kudumisha muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Tupo hapa Kilimani kama wanamichezo kwa maana ya Ofisi ya Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na wenzetu Ofisi ya Rais, wizara ya fedha kule Zanzibar, kila mwaka wakati wa Pasaka huwa tunakutana kama watumishi na kama wanamichezo kwa ajili ya kufanya Tamasha la Pasaka ambapo tunakuwa na michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, netiboli pia, kubwa sana katika mashindano haya ni ushirikiano kati ya sisi tuliopo Tanzania Bara na wenzetu walioko Tanzania Zanzibar,” Amesema Mwenda.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Utumishi na Uendeshaji Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, BSuleiman Mohammed Rashid, mara baada ya kufungua Bonanza hilo, Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Rajab Uweje, ameshukuru Uongozi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara kwa kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar kuimarisha uhusiano kupitia Tamasha la Pasaka linalofanyika kila mwaka.

‘’Tunashirikiana katika masuala ya michezo kama haya kwa ajili ya kuimarisha undugu wetu na kuzidi kufahamiana katika masuala ya kazi, kwahiyo ni kitu kizuri ambacho tunakiendeleza tumekirithi kutoka kwa watangulizi wetu na kina manufaa makubwa sana kwetu sisi tunawashukuru viongozi wetu wa Wizara zetu hizi mbili kwa kuendelea kuimarisha mahusiano haya na yanatusaidia kwa kiasi kikubwa,’’ amesema Uweje.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bonanza la Pasaka ambaye pia ni Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Mgusi Musifa, amesema kwa mwaka huu Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo imefanya maboresho katika Bonanza ikilinganishwa na miaka ya nyuma hususani katika mchezo wa mpira wa miguu kutokana na kuweka timu mbalimbali za nje mbali na timu ya Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.

‘’Tukiongelea histori ya nyuma wakati huu tumeboresha kidogo, kwa sababu kawaida tulikuwa tukicheza sisi Hazina Bara na Hazina visiwani lakini leo tumekuwa na timu sita,’’ ameongeza musifa.

Amesema Tamasha hilo limekuwa likifanyika kwa zaidi ya miaka ishirini sasa na limekuwa likifanyika kwa kuunganisha pande zote mbili za Muungano kwa miaka yote hiyo. Na timu zilizoshiriki ni pamoja na timu ya Maveterani kutoka Bara na visiwani,Police FC, Hazina Sports club, GPSA, PSPTB, Area C na nyingine zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here