Home MICHEZO DK. TULIA AWAJULIA HALI MAJERUHI MASHABIKI WA SIMBA

DK. TULIA AWAJULIA HALI MAJERUHI MASHABIKI WA SIMBA

Na Mwandishi wetu, Chalinze

RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, leo Machi, 30 2024 amefika katika Hospitali ya Msoga iliyopo Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani kwa ajili ya kuwajulia hali Majeruhi wa ajali iliyohusisha gari la Mashabiki wa Simba na Lori la mizigo iliyotokea jana katika eneo la Vigwaza Mkoani humo.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Tulia ametoa mchango wa majeneza mawili kwa ajili ya kuwahifadhi marehemu wa ajali hiyo pamoja na kutoa mchango wa Shilingi Milioni 3 kwa ajili ya kuwasaidia Majeruhi hao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here