Home KITAIFA CHATANDA ATEMBELEA FAMILIA YA BOGOHE MWASISI WA UWT PAMOJA NA CCM MWANZA.

CHATANDA ATEMBELEA FAMILIA YA BOGOHE MWASISI WA UWT PAMOJA NA CCM MWANZA.

Na Mwandishi wetu, Mwanza

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amefika Kisesa wilaya ya Magu mkoani Mwanza kumtembelea Mwasisi wa UWT na CCM Mkoa wa Mwanza Ruth Bogohe kwa dhima ya kuhani msiba wa mziwanda wake Queen Elithabet Joseph ambaye alifariki Machi, 25 2024 na amezikwa Machi 27 mwaka huu.

Ruth ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali
katika uongozi wa awamu ya kwanza wa Hayati Mwalimu Nyerere pamoja na awamu ya pili ya Hayati Ali Hassan Mwinyi Nyadhifa hizo ni pamoja na Katibu Tarafa wilaya ya Mwanza, Diwani wa CCM miaka 15, Mwenyekiti UWT Mkoa wa Mwanza miaka 10 kuanzia Mwaka 1975 hadi Mwaka 1985, Mjumbe Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi miaka 15 kuanzia Mwaka 1977 hadi Mwaka 1992 akiwakilisha Mkoa wa Mwanza.

Pia ni Mama mzazi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Viti 20 Tanzania Bara ambaye pia ni Mjumbe Baraza Kuu UWT Taifa Ellen Makungu Bogohe.

Mhe Chatanda ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Christina Mndeme(MNEC) Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Wajumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa, Viongozi wa UWT Mkoa wa Mwanza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here