Na Esther Mnyika
SERIKALI ya Tanzania na Hangary wamesaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya maji kwa sababu nchi hiyo wanaongoza duniani kwa kudhibiti mafuriko maji taka na maji salama hivyo kupata ujuzi wa teknolojia.
Pia nchi hiyo wanatarajia kufanya uwekezaji wa Kiwanda cha kutengeneza ndege ndogo Mkoani Morogoro.
Akizungumza leo Machi 28 2024 jijini Dar es Salaam baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema ugeni huo umekuja baada ya Rais wa Hangary kufanya ziara nchini mwaka jana.
“Tumefanya mazungumzo ya kiserikali ikiwemo ushirikiano wa kibiashara kufanya makongamano ya kibiashara nchi hizi mbili kufanya ziara za kibiashara kwa sekta binafsi.
” Pia mazungumzo mengine ni kuhusu sekta ya utalii ambapo miaka miwili iliyopita watalii walikuwa 5000 hadi sasa watalii wamefika 11000 ni ongezeko la watalii, “amesema Makamba.
Amesema wanatajia kusaini mkataba wa usafiri wa anga kuwezesha ndege kusafiri moja kwa moja kutoka Hangary hadi Tanzania.
Makamba amesema amesha waahidi kuwapa rasimu ya mkataba huo ili waanze safari hizo mara moja.
Vilevile, wamezungumza namna ya kushirikiana katika elimu watanzania walio nufaika na ufadhili wa masomo 146 amba Nchi ya Hangary ilitoa ufadhili wa masomo 30 na Tanzania tano.
Ameongeza kuwa wanatarajia kufungua uwakilishi nchini ili kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hangary, Peter Szijjàrtò amesema walikuwa na mazungumzo mazuri na nchi hizo mbili zina ushirikiano katika mambo mbalimbali.
“Tulikuwa na mazungumzo tumezungumzia sketa ya maji, elimu, utalii na kuhusu usafiri wa anga tutasaidia nchi ya Tanzania katika sekta hizo na kubadilishana ujuzi na uzoefu kati ya Hangary na Tanzania,”amesema Szijjàrtò.