Home AFYA MDAU WA MAENDELEO NDUGU JOSEPH MUSHI ALIYEJENGA ZAHANAT KIBOSHO AIKOSHA SERIKALI YA...

MDAU WA MAENDELEO NDUGU JOSEPH MUSHI ALIYEJENGA ZAHANAT KIBOSHO AIKOSHA SERIKALI YA CCM

MDAU WA MAENDELEO NDUGU JOSEPH MUSHI ALIYEJENGA ZAHANAT KIBOSHO AIKOSHA SERIKALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Na Ashrack Miraji, Same 

MWENYEKITI  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafii amesema amefurahishwa na kitendo cha Joseph Mushi kuamua kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga zahahati Kibosho itakayokuwa msaada kwa wananchi hao.

Hayo ameyasema Jana Machi 25,2024  Mwenyekiti wa Chama hicho Boisafi Wakati akizindua rasmi Zahanati mpya ya Matela iliyojengwa na mdau wa maendeleo, Joseph Mushi katika kijiji Cha Singa wilayani Moshi mkoani kilimanjaro.

“Niseme familia ya Matela imekuwa ni familia ya mfano wa kuigwa katika Taifa letu,Mambo haya yanafanywa na watu  wachache sana ,hili jambo walilofanya kwa kukamilisha zahanati kwa ajili ya Wananchi wa kijiji hiki na vijiji jirani itakuwa ni historia kubwa na haitoweza kufutika.Wananchi  wataendelea kunufaika na huduma hii ya matibabu katika zahanati hii,” amesema Boisafi.

Amesema  ilani ya CCM wameweka bayana  mambo yatakayofanyika kwa miaka mitano kuanzia 2020  hadi 2025 ikiwa ni pamoja na utoaji huduma ya Afya kwa jamii jambo ambalo limekuwa likipewa kipaumbele kwa nchi nzima na Rais Dk Samia.

Amesema jambo alilolifanya mdau huyo wa maendeleo ni la kuigwa ambalo linaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais  ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na familia hiyo katika masuala huku akitoa wito kwa wananchi wa Kibosho waliopo maeneo mbalimbali waakumbuke kuijenga kibosho.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Msemaji wa familia,Ibrahim Mushi amempongeza na kumshukuru kijana wao kwa  kutimiza  ahadi  yake kwa kushirikiana na serikali ya CCM  kwa kujenga zahanati hiyo itakayowanufaisha wananchi wa kibosho. 

“Niseme tu hii zahanati siyo ya familia ya Matela hii zahanati ni wananchi wote ambao wanaishi maeneo haya na maeneo jirani bila ya kubagua jinsia ya mtu au Dini wala kabila hii zahanat hipo kwa ajili ya Wananchi wote lengo letu ni kumuunga mkono Mhe Rais  Dk. Samia,” mesema  Ibrahim 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here