Home KITAIFA MIAKA MITATU YA RAIS DK.SAMIA TRC YAJIVUNIA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 152.

MIAKA MITATU YA RAIS DK.SAMIA TRC YAJIVUNIA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 152.

Na Esther Mnyika

KATIKA miaka mitatu ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya reli Shirika la Reli Nchini (TRC) linajivunia kukusanya zaidi ya bilioni 152 huku wakitoa wito kwa sekta binafsi kuchangamikia fursa zinazotokana na uwepo ya reli ya SGR.

Hayo ameyasema leo March 25,2024 jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dk. Samia madarakani.

Kadogosa amesema serikali inatengeneza mazingira ya kuziwezesha sekta binafsi kutumia SGR kufanya biashara na nchi nyingine ili kukuza uchumi.

“Bila sekta binafsi reli hii haitakuwa na maana hivyo Watanzania wachangamkie fursa kuinua uchumi wao na katika kipindi cha miaka mitatu shirika hilo limetengeneza zaidi ya shilingi bilioni 152.

“ Mbali na kutengeneza kiasi hicho hatujawahi kutoa gawio lakini tumetoa ‘contribution’ kwani kwa zaidi ya miaka saba tupo katika ujenzi lakini mradi ukikamilika tunatarajia kutengeneza faida,” amesema Kadogosa.

Amesema zaidi ya ajira elfu 31 za moja kwa moja zimetengenezwa kutokana na utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumzia kuhusu changamoto Kadogosa ametaja changamoto walizokutana nazo wakati wa utekelezaji wa mradi huo kuwa ni kuchelewa kufika mahali kutokana na kufuata sheria kwa sababu huwezi kumtoa mtu kwenye eneo lake bila kufuata sheria.

Ameeleza changamoto nyingine ni kimazingira kwani baadhi ya maeneo kuwepo kwa viumbe wasiopatikana eneo lolote hivyo iliwalazimu kutengeneza kwanza eneo la kuwahifadhi kwa mfano eneo la Pugu na Ngelengele.

Ametaja changamoto nyingine ni pamoja na utafutaji wa fedha, uwepo wa mvua nyingi ambazo zilisababisha mradi kuchelewa.

“Kudumu kwa reli yetu itategemea na utunzaji wa mazingira lakini tumetengeneza mradi utakaodumu kwa zaidi ya miaka 100 sasa walinzi wa kwanza tunaowategemea ni wananchi wenyewe,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here