Home KIMATAIFA TANZANIA NA KENYA ZA KUBALIANA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA

TANZANIA NA KENYA ZA KUBALIANA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA

Na Mwandishi wetu,  Kenya

Tanzania na Kenya zimekubaliana na kutia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ili kuruhusu raia kutoka nchi hizo kufanya biashara baina yao kwa urahisi na kwa manufaa ya pande zote mbili.  

Makubaliano hayo yametiwa saini na Wakili Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Stephen Byabato akiwa na mwenzake  Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda kutoka nchini Kenya, Rebbecca Maino. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa Mkutano wa nane wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya katika ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya Machi 22 mwaka huu. 

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya watalaam kisha ngazi ya Makatibu Wakuu ambapo zaidi ya vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru zaidi ya 14 vilijadiliwa na kuwekewa mpango wa kuendelea kuviondoa vyote.

Tanzania na Kenya ni wabia wakubwa wa biashara na hivyo kuondolewa kwa vikwazo hivyo vitasaidia kuongezeka mara dufu kiwango cha kufanyika kwa biashara baina ya mataifa hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here