Home MICHEZO TANZANIA KUANZA MATUMIZI YA VAR KATIKA LIGI KUU BARA.

TANZANIA KUANZA MATUMIZI YA VAR KATIKA LIGI KUU BARA.

Na Mwandishi wetu

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema vifaa vya kiteknolojia kwa ajili ya kuwasaidia waamuzi yani “Video Assistant Referee” (VAR), vitaanza kutumika rasmi katika mechi za Ligi Kuu Bara kuanzia msimu ujao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wallace Karia amesema tayari wameshapokea nyaraka kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa ajili ya kupokea vifaa vya VAR, lakini kabla ya hapo kutakuwa na mafunzo kwa waamuzi ya namna ya kuvitumia.

Karia pia amekaribisha maoni ya kanuni ya kuzikata timu pointi ambazo wachezaji au mashabiki wake wataonekana kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina na kuingia uwanjani wakati mechi inaendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here