Home MICHEZO KARIA NA MANARA WAKUTANA KWENYE IFTAR.

KARIA NA MANARA WAKUTANA KWENYE IFTAR.

Na Mwandishi wetu

MFANYABIASHARA na Mdhamini wa Club ya Yanga Ghalib Said Mohammed (GSM) ameonesha nia ya kuona Rais wa TFF Wallace Karia na Haji Manara wanaelewana baada ya kutofautiana Julai 2 2022 kwenye mechi ya fainali ya Kombe la ASFC lililozikutanisha Yanga na Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Ghalib amewakutanisha Rais Karia na Haji Manara leo jioni katika Iftar iliyoandaliwa na Kampuni ya GSM na kualika Watu mbalimbali akiwemo Naibu Spika, Mawaziri mbalimbali pamoja na Wadau wengine mbalimbali.

Katika picha walizopigwa usiku wa leo Karia na Manara wameonekana wakizungumza, kutabasamu na mwishowe kushikana mikono na kutazama huku wakati wote Mpatanishi GSM akiwa na tabasamu katikati yao.

July 21 mwaka huu wa 2024 Haji Manara atakuwa anatimiza miaka miwili toka afungiwe kujihusisha na soka na atakuwa ana maliza adhabu hiyo ambayo pia ilimtaka alipe faini ya milioni 20.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here