MPENZi wa zamani wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zarina Hassan maarufu The Boss Lady, anatarajiwa kutoa msaada kwa wanawake waliojifungua kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hatua hiyo inakuja baada ya kuongeza mkataba wa ubalozi na kampuni ya Doweicare inayotengeneza ‘Softcare diaper ‘ na taulo za kike.
Akizungumza leo Machi 21 2024 jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari wakati wa kusaini mkataba huo mpya, Zari amejivunia kufanya vizuri kama balozi wa bidhaa za kampuni hiyo na ndiyo sababu ya kuendelea kuitangaza.
Amesema tangu aliposaini mkataba wa kwanza zaidi ya miaka mitatu iliyopita, amefanya vizuri na kuweza kuwafikia watu wengi ikiwamo pia kutoa misaada hasa ya taulo za kike kwa wanafunzi katika shule mbalimbali nchini.
“Nimefanya kazi na kampuni hii muda mrefu, wamefurahi kuendelea kufanya kazi na mimi kwa kuwa ‘brand’ imezidi kukua.Karibia nchi zote za Afrika ambazo bidhaa hizo zinafika, mimi nimehusika kuzitangaza,” amesema Zari.
Katika hatua nyingine ameweka wazi kuhusu uhusiano wake na wanawake wengine wa Diamond kuwa amekuwa akiwasiliana nao vizuri akiwamo Zuchu ambaye ndiye anakaa na watoto wake wanapofika Tanzania.
“Wanawake wote wa Diamond mimi naongea nao. Naongea pia na Zuchu kama watoto wangu wanakuja Tanzania nampigia Zuchu nawajulia hali naweza hata nisimtafute Baba T.
“Kuhusu watoto wa Hamisa Mobeto, Diamond mwenyewe ndiyo ataamua kuwa wajichanganye na wangu au la, mimi sina tatizo akiniambia yule ni mtoto wake anataka kujuana na hawa wangu namkaribisha,” amefunguka Zari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Doweicare, Victor Zhang, amesema wamemuongezea Zari mkataba mpya kwa sababu amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza ‘brand’ yao.
Amesema lengo la kwenda kutoa msaada Muhimbili ni kurudisha kwa jamii kama ilivyo kawaida yao, ikiwa pia ni sehemu ya kuzindua bidhaa mpya ya ‘diaper’ ambayo inaweza kutumika kuanzia mtoto mchanga wa siku moja