Home KITAIFA WANANCHI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KUMUCHAGUA DIWANI SENGEREMA.

WANANCHI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KUMUCHAGUA DIWANI SENGEREMA.

Na Mwandishi wetu,

WANANCHI wa Kata ya Buzilasoga wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wamejitokeza kupiga kura kumuchagua diwani wa Kata hiyo kwenye uchaguzi mdogo.

Uchaguzi huo wa diwani wa Kata ya Buzilasoga umefanyika leo Machi 20 wilayani Sengerema unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa Kata hiyo Devid Shilinde wa ChamaChaMapinduzi (CCM) baada ya kufariki dunia.

Vyama nane vimejitokeza kugombea nafasi hiyo ambavyo ni CCM, NLD,ADC, UPDP, ,SAU ,AAFP, CCK, na Demokrasia Makini.

Mkurugenzi wa uchaguzi Jimbo la Sengerema, Binuru Shekidele amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri huku wananchi wakifuata taratibu zote za kupigaji kura.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here