Home BIASHARA TANTRADE YAPOKEA VIFAA MBALIMBALI VYA BILIONI MOJA

TANTRADE YAPOKEA VIFAA MBALIMBALI VYA BILIONI MOJA

Na Esther Mnyika

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (TANTRADE) wamepokea msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wao kutoka mamlaka ya biashara ya Korea Kusini wenye thamani ya zaidi ya bilioni moja.

Akizungumza baada ya kupoke vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE , Latifa Khamis amesema hayo ni matunda mazuri yanayotokana na ushirikiano wa karibu baina ya nchi hizo mbili.

Amesema msaada waliopokea ni pamoja na komputa mpakato( laptop) 10,Desktop 30,vibanda 500,scana simu 30 pamoja na genereta lenye ukubwa wa kv 60.3.

“Haya ni matokeo ya ushirikiano wetu tulifanya mazungumzo ya namna ya kuboresha maonesho yetu ili wafanyabiashara wengi zaidi waweze kushiriki na tuwahudumie kwa ufanisi mkubwa na haya ndio matokeo kwani msaada huu hauna masharti yeyote,”amesema Latifa.

Aidha ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushiriki kwenye maonesho 48 ya biashara ya sabasaba kwani yatakuwa ya aina yake kutokana na vifaa ambavyo wamekabidhiwa kutoka Korea Kusini.

Amesema wadau wa maonesho wamekuwa wakiongezeka wakihitaji kushiriki lakini wamekuwa wakikosa nafasi hivyo kupitia vibanda walivyokabidhiwa watapafa fursa ya kushiriki lakini mapato ya nchi kuongezeka uchumi kukua kupitia TANTRADE.

“Maonesho yanayokuja ya 48 ya sabasaba yataimarika na yatakuwa yenye mvuto zaidi hivyo wadau wote msikose kushiriki na tutawahudumia kwa ufanisi mkubwa”,Amesema Ratifa.

Kwa upande wake Balozi wa Jamuhuri ya Korea Kusini nchin, i Kim Sun Pyo ametoa rai kwa Watanzania kuwekeza zaidi nchi Korea kwani kumekuwa na ushirikiano wa karibu baina ya nchi hizo.

Amesema kufutia mazingira mazuri ya uwekezaji na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo wameahidi kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha ufanyaji wa biashara baina ya nchi hizo unaimarika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here