Home KITAIFA KAMATI YA BUNGE YA PIC YAITAKA SERIKALI  KUIWEZESHA TBA 

KAMATI YA BUNGE YA PIC YAITAKA SERIKALI  KUIWEZESHA TBA 

Na Mwandishi wetu 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC) imeka Serikali kuiwezesha Wakala  Majengo Nchi (TBA).

 Hayo yamesemwa  leo Machi  20 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti na Kamati hiyo  Deus Sangu  wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi katika eneo la Magomeni Kota awamu ya pili  amesema kuwa TBA imefanya uwekezaji wenye tija.

“Katika kikao chetu na Menejimenti ya TBA tumepata fursa ya kuoneshwa mpango wa ujenzi wa majengo ya makazi katika eneo hili la Magomeni Kota ambapo tumeshuhudia jengo moja limekamilika na jengo la pili likiwa limefikia 96%,” amesema  Sangu.

Vile vile  amepongeza uwekezaji huo uliofanywa na TBA kuwa unakwenda kutatua changamoto ya makazi kwa wakaazi mbalimbali wa jiji la Dar es Salaam kwa kupata makazi ya uhakika.

Pia ameitaka Serikali kuhakikisha inatoa fedha kwa wakati  ili kukamilisha mpango huo wa ujenzi wa majengo matano katika eneo hilo la Magomeni Kota kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa makazi kama ilivyokusudiwa.

Aidha,  ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na  Rais Dk.  Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuruhusu kufanyika uwekezaji ambao unagusa wananchi wa hali zote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TBA Arch. Dk. Ombeni Swai ameishukuru Kamati kwa kufanya ziara hiyo na kuahidi kuendelea kuisimamia Menejimenti ya TBA katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here