Home KITAIFA TRILIONI 2.53 ZAIPAISHA TARURA NDANI YA MIAKA MITATU YA MHE.RAIS SAMIA,MAMEYA WA...

TRILIONI 2.53 ZAIPAISHA TARURA NDANI YA MIAKA MITATU YA MHE.RAIS SAMIA,MAMEYA WA KINONDONI NA ILALA WAFURAHISHWA NA MRADI WA DMDP

Na Catherine Sungura, Dar es Salaam

KATIKA kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, bajeti ya kuboresha miundombinu chini ya TARURA takribani trilioni 2.53 zimepokelewa kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara za vijijini na mijini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa wakati akielezea mafanikio ya miaka mitatu ya Rais lDmkoani Dar es Salaam.

Amesema nyakati ambayo Serikali imefanya kazi kubwa upande wa miundombinu ni kipindi cha Awamu ya Sita ndio maana Rais aliliona hilo na kuongeza bajeti ya TARURA.

Amtaja mafanikio ya ujenzi wa barabara za lami na miradi ya kimkakati, zimejengwa barabara za Lami kilomita 819.22 ambazo zimeongeza mtandao wa barabara za lami toka kilomita 2,404.90 hadi kilomita,224.12.

“Wakati wa Baba wa Taifa alipoanzisha msingi wa kukuza miji kupitia dhana ya ujamaa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dk. Samia imeendeleza misingi ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere,” amesema Mchengerwa.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara za changarawe Mchengerwa amesema kilomita 11,924.36 zimejengwa na kuongezeka mtandao wa barabara za changarawe toka kilomita 29,183.17 hadi kilomita 41,107.52 na ujenzi wa Madaraja Wakala imejenga madaraja makubwa sita (6) ambayo ni ya Berega (140m) -(Kilosa,) Msadya (60m) -(Mpimbwe DC), Mwasanga (40m)- (Mbeya) yamejengwa na yanatumika.

“Rais amewagusa wananchi wengi wa vijijini kwa ujenzi wa madaraja ya Kiwila-(40m)-Ileje, Mkomanzi-Korogwe (60m) na Kalambo (80m)-(Kalambo) ujenzi ambao unaendelea kukamilishwa, tunawapongeza TARURA chini ya Mtendaji Mkuu Mhandisi Victor Seff,”amesema

Aidha, ametaja mafanikio mengine ni ujenzi wa barabara na madaraja kwa kutumia malighafi za ujenzi zinazopatikana maeneo ya kazi zinapotekelezwa kama mawe, matofali ya kuchoma, ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe.

“Hadi sasa jumla ya kilomita 23.18 za Barabara ya Mawe zimejengwa kwa gharama ya bilioni 8.1 ambapo ni sawa na bilioni 12.8 kama tungetumia lami nyepesi (double surface dressing) na bilioni 33.6 kama tungetumia lami ya zege (Asphat Concrete),”ameongeza.

Vilevile amesema ujenzi wa madaraja kwa kutumia mawe ni mojawapo ya kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.

Pia amesema hadi Mwezi Februari, 2024 TARURA imejenga madaraja 226 ya mawe yenye thamani ya bilioni 12.52 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Wakala unaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.

Hadi sasa kwa kutumia Teknolojia ya ECOROADS zimejengwa Km 22 na ujenzi upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.

Naye, Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto alisema ndani ya miaka mitatu mradi wa DMDP kwa wilaya ya Ilala umeweza kuondosha kero za barabara kwa wakazi wengi wa Ulongoni hadi Gogolamboto ambao awali walijiona wametengwa.

Amesema walipata bilioni 17.6 kwa ajili ya ujenzi wa barabara na mifereji na hivyo kuweza kuondoa changamoto na kuifanya Ilala kufunguka.

Kwq upande wake Naibu Meya wa Kinondoni, Joseph Rugasira amesema DMDP-1 walipata ujenzi wa barabara Km 55 na mitaro zaidi ya Km 8.9 na kufanya maeneo mengi ya Mwananyamala, Tandale na Kinondoni kwa ujumla kupendeza.

“Tunampongeza Rais kwani DMDP-2 itaenda kutatua changamoto za barabara na wananchi wanafurahia kuona maendeleo katika miundombinu, ”amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here