Home KIMATAIFA RAIS DK. SAMIA AKUTUNA NA RUTO NA MSEVENI ZANZIBAR

RAIS DK. SAMIA AKUTUNA NA RUTO NA MSEVENI ZANZIBAR

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wageni wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya walipowasili Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar 14 Machi, 2024.

Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation). Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here