Home BURUDANI Halima amesema urembo unahitaji uwekezaji kama sekta zingine

Halima amesema urembo unahitaji uwekezaji kama sekta zingine

Na Mwandishi wetu

Mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Mrembo wa Dunia(Miss World 2024)Halima Kopwe ameimba serikali kuwekeza kwenye tasnia ya urembo kama inavyofanya kwenye mpira kwani itasaidia kuendelea kuitangaza nchi lakini pia kuvutia vijana wengi kuingia kwenye tasnia hiyo.

Hayo ameyasema leo March 13,2024 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ishiriki wake kwenye mashindano hayo.

Tasnia ya urembo inahitaji uwekezaji kama kwenye tasnia nyingine ili hata ikitokea mashindano ya kimataifa iweze kuiwakilisha vyema nchi.

“Sisi kama nchi tunakila kitu maana hata nilivyoshiriki haya mashindano ya Miss World sijaona kitu kikubwa ambacho kama nchi hatuwezi kufanya sema wenzetu wamewekeza sana unakuta mtu vazi la ubunifu anavalishwa na mbunifu mkubwa wa nchi husika tofauti na sisi mpaka utafute mwenye mimi naamini serikali ikiwekeza kwenye tasnia hii kama wanavyofanya kwenye mpira tutafuka mbali”Amesema Kopwe.

Amesema ameweza kuiweka nchi kwenye rekodi nzuri baada ya kuingia kwenye kumi bora kupitia project yake ya Damu yangu kizazi changu yenye lengo la kumsadia mwanamke mjamzito na mtoto.

Amesema kupitia project hiyo ameweza kuingia kwenye 10 bora lakini pia kurudisha ushindi wa kuingia kwenye 40 bora ambapo ushindi huo kama nchi uliupata mwaka 2005.

Sambamba na hayo ametoa rai kwa wadau pamoja ya kuwa project hiyo ipo chini taasisi ya miss Tanzania bado inahitaji kuendelea kuisaidia jamii yake kama sehemu ya maisha yake ameomba wadau kumsapoti ili apate gari la wagonjwa kwa ajili ya kupeleka gari hilo katika mkoa wa Mtwara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ukuzaji na maendeleo ya sanaa baraza la taifa la sanaa(BASATA) ameipongeza kamati ya Miss Tanzania kwa kuweza kumsimamia mrembo huyo mpaka kuiletea nchi heshima hivyo wameahidi kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha tasnia ya urembo inaendelea kuiwakilisha nchi kwenye mataifa mengine.

Naye,Muwakilishi wa mkurugenzi wa kampuni ya The look Bi.Halima Mhando amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameitendea haki tasnia ya urembo na sanaa kwani hata mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia uwekezaji mkubwa anaoufanya lakini pia kuitangaza nchi kupitia filamu ya The Royal Tour ambayo imefanya nchi kujulikana kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here