Home AFYA Halmashauri 112 kati ya 119 nchini hazina maambukizi mapya ya Matende na...

Halmashauri 112 kati ya 119 nchini hazina maambukizi mapya ya Matende na Mabusha

Na Mwandishi wetu 

Waziri wa Afya,  Ummy Mwalimu amesema nchi imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha inatokomeza magonjwa ya matende na Busha kwa kuokoa watu milioni 31.2 waliokuwa na hatari ya kupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo.

Akizungumza  leo Machi 12 Jijini Dar es salaam na waandishi wa Habari  wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kutokimeza ugonjwa huo nchini hususani mkoa wa Dar es salaam.

Amesema awali maambukizi makubwa ya ugonjwa huo yalikuwa katika  Halmashauri 119 ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wameza kudhibiti ugonjwa huo katika Halmashauri 112 kati 119 na kubakiwa na Halmashauri 7.

“Mkoa wa Dar es salaam Halmashauri zote yaani ya manispaa ya Kigamboni na Ubungo,Temeke na Halmashauri ya jiji hazina maambukizi mapya ya ugonjwa huu baada ya kusitisha umezeshaji wa kinga tiba na kubaki na kata 10 za Halmashauri ya Kinondoni ambazo zinamaambukiza mapya kwa asilimia 2.3.

“Kutokana na matokeo haya wizara ya Afya inapenda kutoa taarifa rsmi kwa wananchi wa mkoa huu tunasitisha kampeni za uwezeshaji wa kingatiba ya ugonjwa lakini pia nitoe rai kwa wananchi kuchukua taadhari kwa kufanya usafi na kuua mazalia wa mbu,” amesema Ummy.

Amesema zoezi la umezeshaji kingatiba unafanywa kwa kata 10 za manispaa ya Kinondoni ambazo ni Tandale,Kijitonyama,Mwananyamala,Kigogo,Mzimuni,Magomeni,Ndugumbi,Hananasif, Kinondoni na Makumbusho.

 Ummy ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni hiyo ya kingatiba zitakazoendelea kufanyika kwenye maeneo yao ili kuweza kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo.

Pia amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono jitihada za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa ayapewi kipaumbele.

“Kupitia mkutano wa ‘Reaching the last mile’uliofanyika mwezi Desemba 2023 huko Dubai Rais  aliahidi kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani milioni tatu katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2024 ili kufanikisha kutokomeza magonjwa haya  hususani Matende na Mabusha,”amesema.

Ametaja Halmashauri zenye maambukizi mapya hivi sasa ni Pangani, Mafia, Kinondoni, Kilwa, Lindi Manispaa, Mtama na Mtwara Mikinfani ambako kuna jumla ya wakazi 1,203,359.

Kwa upande wake wake Mratibu  wa Udhibiti  wa Ugonjwa  wa Matende  n Busha Wizara ya Afya, Dk. Faraja Lyamuya amesema sababu zinazo changia maambukizi mapya kati6 baadhi ya maeneo  ni jamii  kutokuwa na uelewa wa kutosha pamoja na kuhamahama hatua inayosababisha kutoshiriki kikamilifu katika umezaji wa kingatiba 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here