Home BURUDANI STEVE NYERERE AMESEMA WANATARAJIA KUAANDAA TAMASHA KUBWA

STEVE NYERERE AMESEMA WANATARAJIA KUAANDAA TAMASHA KUBWA

Na Mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele maarufu kama”Steve Nyerere” amesema wanatarajia kufanya  Tamasha kubwa kwaajili  ya walemavu  nchini na kuwapatia mahitaji muhimu mbalimbali ikiwemo wheelchair. 

Akizungumza leo Machi 11 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari  Mwenyekiti huyo amesema lengo la taasisi hiyo ni kusaidia jamii  na wanafanya kazi na makundi mbalimbali. 

Amesema lengo la Tamasha hilo ni kusoma dua kwaajili ya  nchi kuendelea kuwa kisiwa cha amani na watu wote waliotangulia mbele za haki.

“Taasisi hii imefanya mambo mengi kwenye jamii  na kusaidia  ikiwemo kuwapatia watoto vifaa vya shule, sare na viatu kwa wanafunzi,” amesema Steve. 

Amesema katika Miaka mitatu ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wataungana na makundi mbalimbali kusaidia jamii Wamezindua rasmi leo kauli mbiu  yao “mtonye mwenzako mama tena”

Ameongeza kuwa kila  mwezi  watakuwa wanatoa tathimini ya taasisi hiyo.

Kwa upande wake Susan Lewis maarufu kama Mama Natasha amesema Taasisi hiyo inajumuisha wasanii mbalimbali ambao wanalenga  kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kusaidia vifaa vya shule vua watoto .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here