Home KITAIFA FCC YAZINDUA MAADHIMISHO SIKU YA KUMLINDA MLAJI DUNIANI

FCC YAZINDUA MAADHIMISHO SIKU YA KUMLINDA MLAJI DUNIANI

Na Mwandishi wetu

TUME ya Taifa ya Ushindani Nchini (FCC) imezindua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Kumlinda Mlaji Duniani ambayo imelenga kutoa elimu ya masuala mbalimbali kuhusu haki za mlaji ,mtumiaji na haki za usalama wa mlaji, kuchagua, kupata taarifa ya bei, ujazo pamoja malighafi zilizotumika katika bidhaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2024 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio, amesema kuwa kilele cha maadhimisho Siku ya Mlaji Kitaifa itafanyika Machi 15, mwaka huu katika Hoteli ya Protea Upanga jijini Dar es Salaam,

Amesema mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Ashantu Kijaji,ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ‘Matumizi ya akili mnepa yanayozingatia haki na wajibu wa mlaji’

“Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Kumlinda Mlaji Kitaifa kutakuwa na kongamano pamoja na mada mbalimbali zenye lengo la kujenga uwelewa mkubwa” amesema Bw. Erio

Ameongeza kuwa tangu Machi 8, 2024 walianza kuadhimisha siku ya Kumlinda mlaji kwa kutoa elimu kupitia Ofisi za FCC zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma Mwanza pamoja na Arusha.

“Machi 13, 2024 tutakuwa na kliniki na walaji katika ofisi za FCC Mko wa Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto pamoja na kutoa maelekezo namna bora ya kutatua changamoto hizo,” amesema Erio.

Amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa kwa kushiriki kliniki hiyo kwaajili ya kupata elimu na majibu ya hoja katika maeneo mbalimbali ambayo wengependa kujua kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo.

Uzinduzi wa siku ya kumlinda mlaji dunia ulianzishwa mwaka 1980 na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo na kutengeneza kanuni za kumlinda mlaji.

Umoja wa Mataifa walianza kuadhimisha siku ya kumlinda mlaji dunia Mwaka 1983 ambayo inafanyika Machi 15 kila mwaka ambapo Tanzania ilianza rasmi kuadhimisha siku hiyo mwaka 2009.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here