Home KITAIFA WAVUVI WA PWEZA MKINGA WACHEKELEA KUVUA TANI 2.5 KWA SIKU, MWAMBAO,NORAD WAAHIDI...

WAVUVI WA PWEZA MKINGA WACHEKELEA KUVUA TANI 2.5 KWA SIKU, MWAMBAO,NORAD WAAHIDI NEEMA ZAIDI.

Na Boniface Gideon, MKINGA

WAVUVI wa Samaki aina ya Pweza kutoka Vijiji vya Boma Kichakamiba,Boma Subutuni na Moa wameweka historia baada ya kuvua Kilogram.2284 kwa siku moja ambazo ni sawa na tani 2.2,Huku kila mvuvi akiwa na wastani wakuvua zaidi ya Kilogram.40 kwa siku,

Akizungumza Machi 9 Mkoani Tanga wakati wa hafla ya kufungua Mwamba wa Pweza wa Chundo uliofungwa kwa siku 90, Katibu wa Jumuiya ya Usimamizi Bahari ( BMU )Kata ya Boma, Ukasha Malumbo amesema awali, kabla ya kupatiwa elimu ya mazingira na usimamizi bora wa rasilimali bahari wavuvi wa pweza walikuwa wanavua chini ya kg 3 na walikuwa hawafanyibiashara.

Amesema wingi huo wa Pweza umetokea mwisho mwa wiki katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga matokeo ya Elimu ya utunzaji wa mazingira kutoka Shirika la Mwambao Coastal Community Network chini ya mradi wa NORAD.


“Elimu hii kwa wavuvi inahusisha utunzaji wa matumbawe ambayo ndio makazi ya Samaki,ufungaji wa miamba bahari ili kuruhusu Samaki kuzariana na kukua kwa siku 90 kwenye kila mwamba, upandaji miti aina ya mikoko, utunzaji wa fukwe, utoaji wa vitendea kazi kama vile Boti za Uvuvi na Mitaji.

“Mwanzo sisi wavuvi tulikuwa tunavua tu ilimradi tupate mboga,hakuna mvuvi aliyewahi kuvua hata kilogram 10 ,lakini walipokuja wafadhiri walitupatia elimu ya utunzaji wa mazingira usimamizi bora wa rasilimali bahari na faida za kufunga miamba bahari na tukajaribu kwa mara ya kwanza mwaka 2022 ambapo mvuvi wa juu kwa siku moja alikuwa na wastani wakuvua zaidi ya kilogram 50 na wachini alipata kilogram 17 na kilogram 1 tunauza shilingi7000 ambapo Shilingi 1000 inakatwa ya BMU na Halmshauri , hivyo mvuvi anapata shilingi 6000 kwa kila kilogram moja ya Pweza,” Amebainisha Malumbo

Ametaja baadhi ya changamoto kubwa zinazowakabili wavuvi hao ni upungufu wa vitendea kazi kama boti zakufanyia doria dhidi wavuvi haramu pamoja na baadhi ya wavuvi kutokukubaliana na elimu ya utunzaji wa matumbawe na ufungaji wa miamba bahari ili kuruhusu samaki kuzariana,

” Tunakabiliwa na changamoto kubwa ya Upungufu wa Boti za mwendo kasi kwaajili yakufanya doria , uvamizi wa miamba bahari kutoka kwa baadhi ya wavuvi hususani kutoka vijiji vya jirani ambapo wanakuja kuvua kwenye miamba tuliyoifunga,”amesema.

Akitoa matokeo ya zoezi la upimaji wa samaki aina ya pweza Msimamizi wa Mradi wa Utunzaji wa Rasilimali Bahari kutoka Shirika la Mwambao Coastal Community Network chini ya ufadhiri wa NORAD , Willy Moses amesema zaidi ya kilogram 2284 ambazo ni sawa na tani 2.2 zimevuliwa kwa siku moja ikiwa ni ongezeko kubwa ambapo mara ya mwisho walifanikiwa kupata kilogram 1600 kwa siku 3 za zoezi hilo.

“Kwa leo hii peke tumefanikiwa kupata zaidi ya tani mbili ambapo Kuna baadhi ya Wavuvi wamevua zaidi ya kilogram 50 hivyo haya ni matokeo makubwa katika harakati zetu za utoaji wa elimu ya tunzaji wa rasilimali bahari na uwezeshaji wa vitendea kazi,” amesema Willy.

Amesema Wavuvi wamewezeshwa kuanzia elimu ya utunzaji wa rasilimali bahari,vifaa vya uvuvi na mitaji kwa wavuvi na wajasiriamali pamoja na wateja wakununua pweza kupitia Jumuiya ya Usimamizi Bahari ( BMU ) .

“Tunafunga miamba kwa siku 90 na kila mwamba utavuliwa kwa siku 3 kwa kawaida samaki aina ya pweza anakuwa mkubwa kwa miezi mitatu, hivyo tumewatafutia soko kupitia makampuni ya ununuzi wa samaki ambapo tunawashindanisha na anayeshinda ndiye anayenunua,na kwa zoezi hili kilogram 1 inauzwa kwa shilingi 7000,” amesema.

             

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here