Home KITAIFA watumishi wa nishati watoa elimu ya nishati safi.

watumishi wa nishati watoa elimu ya nishati safi.

Na Mwandishi wetu,Dodoma

WANAWAKE wa Wizara ya Nishati, wameungana na wanawake wenzao dunia kuadhimisha siku ya wanawake ambayo Mkoani Dodoma imeadhimishwa wilayani Chamwino.

Katika madhimisho hayo watumishi wametumia siku hiyo kuelimisha wananchi mbalimbali kuhusu nishati safi ya kupikia.

Akitoa elimu kwa baadhi ya wananchi Joyce Msangi afisa Misitu, amesema utumiaji wa nishati safi ya kupikia unalinda afya za walaji na inamuepusha mtumiaji na madhara mbalimbali

Amebainisha madhara hayo, ni pamoja na adhari kwenye mfumo wa upumuaji na inaharibu mazingira yanayotuzunguka.

Naye Afisa Kumbukumbu, Talkisia Erio amewahimiza wanawake wa Dodoma kutumia nishati safi ya kupikia ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Kwasababu matumizi ya nishati safi ya kupikia yanauwezo wa kuhudumia watu wengine kwa muda mchache na kufanya mambo mengine ya kujikwamua kiuchumi,” amesema.

Ameongeza kuwa wanawake hao wamewashukuru watumishi hao na kuahidi kwenda kufanyia kazi elimu hiyo waliyoipata.

Katika Madhamisho hayo, yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Chinagali Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here