Home KITAIFA profesa Mkenda mtaala mpya wa mafunzo umeanza kutumika mwaka huu.

profesa Mkenda mtaala mpya wa mafunzo umeanza kutumika mwaka huu.

Na Mwandishi wetu

Waziri wa elimu,sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mtaala mpya wa mafunzo imeaanza kutumika mwaka huu ngazi ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu.

Pia mitaala mipya imeanza wanaosoma darasa la tatu la sasa wataishia la sita.

Hayo ameyasema leo March 7,2024 jijini Dar es salaam kwenye kikao cha mafunzo ya mataala mpya kwa wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali ya habari nchini lengo likiwa kuwajengea uelewa kuhusu mtaalam mpya ili waweze kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vyao vya habari.

Amesema mtaala huo utasaidia watoto kujifunza kwa vitendo ambapo mtoto anapotoka shule anakuwa na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa.

“Mtaala huu umeanza kwa shule za wali,darasa la kwanza na la tatu ambapo shule ya awali mtoto atasoma kwa mwaka mmoja na kuingia darasa la kwanza ambapo atahitimu darasa la sita na kulazimika kusoma mpaka kidato cha nne kwa amri.(lazima),”amesema Profesa Mkenda.

Amesema mabadiliko hayo ni utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la mwaka 2023 ambayo inabainisha mwisho wa elimu ya msingi ni darasa la sita.

Profesa Mkenda, Ameeleza kuwa mabadiliko ya mitaala yameanza mwaka huu yakihusisha ngazi ya darasa la kwanza na la tatu upande wa sekondari tumeanzia kidato cha kwanza kwa shule za mkodo wa Amali na mabadiliko hayo yatahusisha kidato cha tano na vyuo vya ualimu.

“Mtaala huu unamtaka mtoto kusoma kwa miaka 10 kwa lazima ni lazima mtoto amalize kidato cha nne kwa amri,”mesema.

Vilevile amesema wanafunzi wa darasa la tatu kwa sasa ikifikia mwaka 2027 watakuwa darasa la sita na ndio mwisho wale wa darasa la nne la sasa wao watakuwa darasa la saba la mwisho kwa mtaala wa zamani.

Amesema kuwa katika mtaala huo mtoto atasoma masoma ya amali na kawaida yaani mtoto atachagua ambapo mafunzo ya amali mtoto akimaliza shule anaweza kujiajiri.

Ameongeza kuwa katika mtaala huo mpya umeeleza mtoto kufundishwa somo la ujasiliamali hivyo walimu wa somo hilo wanaandaliwa ambapo sasa wameanza kwa mkondo wa elimu ya amali pekee.

“Kwa watoto watakaosoma amali watakapoenda elimu ya juu watasoma miaka mitatu na wakimaliza watapata cheti cha kuhitimu lakini pia cheti cha Veta,”amesema.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, ProfesaCaloryne Nombo amesema utekelezaji wa mtaala huo unaenda sawa maboresho ya sera ya elimu.

Amesema utekelizaji wa sera hiyo ulikua shirikishi kama maagizo yalivyotolewa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kutaka sera hiyo ipitiwe kwa miaka miwili huku ikishirikisha majadiliano ya wadau mbalimbali.

“Tumefanya majadiliano na jamii ya kitanzania kuhusu sera hiyo na baadae ikaidhinishwa na baraza la mawaziri hivyo tunawaomba wanahabari mtusaidie kutoa elimu ya mtaala mpya kwa jamii kwani tumaamini mnanguvu kubwa ya ushawishi katika kuifikia jamii,” amesema Prof Nombo.

Sera ya elimu imejikita katika katika maeneo 7 ambayo ni Mfumo wa elimu na mafunzo,fursa za elimu,ubora wa elimu na mafunzo,Rasilimali watu,usimamizi na uendeshaji,mfumo wa ugharamiaji na masuala mtambuka.

Aidha mtaala huo utazingatia kulea na kuendeleza vipaji na vipawa katika mfumo wa elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here