Home MAKALA Happiness amewataka wanawake kuchangamkia fursa AfCFTA

Happiness amewataka wanawake kuchangamkia fursa AfCFTA

Na Mwandishi wetu,

Mkurungenzi wa Kampuni ya Aja T.L ambaye ni Kinara katika kufanya biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA), Happiness Nyiti amewahimiza wanawake kufanya biashara katika soko hilo.

Akizungumza na Lajiji Media Machi 8 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani amesema yeye ni mmiliki wa kampuni mbili ambayo ni Tanznia Sisal Fiber co limited iliyopo nchi ya Morocco ambayo inajihusisha na uuzaji wa nyuzi za Mkonge zinazotumika katika oganic house building materials.

Amesema wanawake wanapaswa kuwa na uthubutu wa kufanya biashara katika soko hilo kwa sababu kuna fursa nyingi ambazo zinapatikana katika soko hilo .

“Juhudi anazofanya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua fursa katika mataifa mbalimbali ikiwemo Eneo Huru la Biashara Afrika hii ni kwaajili yetu wanawake ambao tunajishughulisha na biashara,Mama Samia amefungua milango ili tuweze kufanyabiashara zetu Afrika,”amesema Happiness.

Amesema kwa sasa wanatafuta wanawake ambao wapo tayari kuingia katika soko hilo ili kutengeza msingi wa pamoja ambao utawawezesha kujua taratibu ya kufanya biashara nje ya nchi ikiwemo sheria mbalimbali na fursa zilizopo.

Amesema kuwa katika Eneo Huru la Biashara Afrika ni moja ya watu waliofaidika kufanya biashara katika soko hilo hivyo amewataka wanawake kuwa na bidhaa zenye ubora na kukidhi vigezo ambavyo vinahitajika kimataifa.

Happiness ameeleza kuwa katika soko hilo kuwa na uhakika wa bidhaa na usambazaaji wa bidhaa hizo kwa wakati ili upatikanaji uwe rahisi kwa mteja anapohitaji bidhaa na anapata kwa wakati bila changamoto yeyote.

Anasema katika uuzaji wa bidhaa katika soko hilo bei zinakuwa za ushindani kwa lengo la bidhaa zao ziweze kuuzika kwa urahisi na kwa uharaka zaidi.

“Kwa sasa hivi wanawake wa Tanzania kuna fursa kubwa kwasababu Waziri wa Viwanda na Biashara,DK.Ashantu Kijaji ni Mwenyekiti wa Mawaziri walio chini ya mkataba wa Soko hili ni Dhahiri wanawake tunaweza kufanyabiashara katika soko hili,”amesema.

Amesama kwa sasa hali ya biashara katika soko hilo ni nzuri na milango iko wazi wanawake wanatakiwa kuamka kwa karne waliyopo ni ya kujishughulisha na biashara kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na kuchangia Pato la Taifa.

Happiness anasema kuna mnyororo wa thamani ambao wanawake wengi wapo humo ndani ambao wanawawezesha wanawake wenzao kufanya biashara kuvuka mipaka katika soko hilo mfano katika biashara ya mkonge wanawake wanahusika katika kuchambua, kupanga, kuandaa nyuzi za Mkonge ni ongozeko la ajira kwa wanawake.

Amesema Tanzania kuna rasilimari nyingi ambazo nchi nyingine hazina kuna fursa za mazao ya kilimo,madini, misitu na sanaa na ubunifu hivyo mwanawake wanapswa kutumia fursa hizo kuuza bidha zinatokazo na rasamali.

“Wanawake wakizalisha bidhaa ziitokanazo na rasmali zetu tunaweza kuuza bidhaa zetu kwa wingi katika soko hili furs ni kubwa inapasa kutumia fusra hizi kwa sababu Rais DK. Samia ametengeneza mazingira rafiki ya ufanyanyi biashara nje ya mipaka ya Tanzania,”amesema.

Amesema sio tu kupeleka bidhaa katika nchi zilizopo kwenye Eneo Huru la Biashara Afrika pia wanafursa ya kuingiza bidhaa za nje ya nchi ambazo zipo kwenye makubaliano ya soko hilo hivyo fursa muhimu kwa wafanyabiashara wanawake nchini.

Amefafanua kuwa wanawake ndio nguzo wakifanya vizuri katika soko hilo kuwawezesha vijana kuingia katika soko hilo kwa urahisi na kuwasaidia kuwapa elimu, ujuzi na kuwashika mkono hiyo itaongeza ajira kwa vijana wanaotoka vyuoni na wanaonza biashara kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Happiness amesema kutoka na uhitaji wa soko hilo watawawezesha wajasiriamali kutengeneza bidhaa zinazo kidhi viwango kutengeneza soko ambalo watanufaika nalo.

“kutoka na mitaji yetu kuwa midogo amawataka wanaweke kuungana katika vikundi ili iwe rahisi kufanya biashara kwa urahisi na kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa katika soko hili itakuwa tumesaidia kuinua Uchumi wanchi yetu,”amaesema.

Amesema umoja wetu kama wanawake ndio utakao wapeleka mbele zaidi katika soko hilo wakishirikiana na kusaidiana katika mambo mbalimbali, wakati huo sio wa kujaribu ni kufanya kwa kutenda na wamefikia ngazi ya uongozi na kuna wanawake wafanyabiashara wakubwa.

Aidha amesema wanawake kutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zao katika soko hilo utumiaji mzuri wa mitandao hiyo huleta fursa katika soko.

Ameongeza kuwa waanawake wanatakiwa kufanyakazi hatakama hakuna mtaji wa biashara wafanyakazi ambayo itawaingizia kipato kwa siku hawawezi kuajiriwa wote lazima wajitume kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao na changamoto wanazokutana nazo ndio fursa wakiangalia kwa jicho chanya wasikatee tamaa.

“Wekeza katika kufanyakazi au kutengeneza bidhaa nzuri ambayo itauzika sokoni sio kuangalia pesa kwanza kabla hujawekeza kwenye bidhaa ambayo itawavutia wateja na kuwajengea imani wateja kwa bidhaa yako ,”amesema.

Amewashauri wanawake kuchangamkia fursa zinapotokea kwa wakati na kutafuta taarifa sahihi katika fursa hiyo na pia wasijiwekee kipimo katika kujifunza mambo mapya maana ni hazina na kuto kuchagua aina ya kazi au kuangalia ngazi ya elimu aliyonayao katika kufanya kazi au biashara.

Happiness ameishukuru wizara ya viwanda na biashara kwa ushirikiano na juhudi wanazofanya kunyanyua wanawake na kuwapatia fursa zitakanazo na soko hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here