Home KITAIFA Rais Dk.Mwinyi Atoa Shukurani.

Rais Dk.Mwinyi Atoa Shukurani.

Na Mwandishi wetu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa shukrani kwa Wakuu wa Mikoa yote mitatu Unguja kwa kuandaa Khitma ya kumrehemu Baba yake mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassani Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29 2024, Dar es Salaam na kuzikwa Machi 2 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Machi 7 katika Khitma na Dua Maalum ya kumwombea Hayati Mzee Mwinyi iliyofanyika Kombeni, Mkoa wa mjini Magharibi, Unguja.

Amewashukuru Masheikh, Viongozi wa Serikali, Dini na wananchi kwa uwepo wao katika khitma mbalimbali zinazoendelea kufanyika Zanzibar

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here