Home KITAIFA Rais Dk.Mwinyi ajifunza mengi kutoka kwa Hayati Mzee Mwinyi

Rais Dk.Mwinyi ajifunza mengi kutoka kwa Hayati Mzee Mwinyi

Na Mwandishi wetu, Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametaja baadhi ya mambo aliyojifunza kutoka kwa Rais Hayati Ali Hassan Mwinyi wakati wa uhai wake.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Machi 5 2024 Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakati wa Dua ya khitma iliyofanyika kwenye Msikiti wa Zinjibar Mazizini ulioandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwaajili ya kumuombea aliyekuwa Rais Hayati Mzee Mwinyi.

Amesema Hayati Mzee Mwinyi alikuwa na Subira kubwa wakati alipokuwa kiongozi hususan kipindi cha mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi.  Watu walimsema vibaya kwa mambo ya kutunga katika vyombo vya Habari lakini hakuwahi kumjibu  yeyote kwa mabaya waliyomsema.

“Alhaj. Dk. Mwinyi mimi nimejifunza kusubiri kwa fundisho alilolipata kwa Mzee wake kwa kumpa mafunzo mema,”amesema Dk.Mwinyi.

Amesema wakati Hayati baba yake alipokuwa akitibiwa Uingereza aliwataka madaktari na familia arudishwe nyumbani na baadae apelekwe Zanzibar, maneno hayo aliyarudiarudia hata baada ya kufika Dar es Salaam.

Rais Dk. Mwinyi ameishukuru kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mazishi inayoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla pamoja na wajumbe wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here