Home BURUDANI Zuchu afungiwa miezi sita Visiwani Zanzibar

Zuchu afungiwa miezi sita Visiwani Zanzibar

Na Mwandishi wetu 

BARAZA la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, ( BASSFU), limemfungia msanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu kwa jina la Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita.

Aidha BASSFU  limepiga marufuku redio na televisheni za visiwani humo kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi hicho.

Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la hivi karibuni Zuchu akiwa jukwaani kwenye Tamasha la Full Moon Party akitumbuiza na alitoa matamshi na kuonesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya Kinzanzibari.

Baada ya tamko hilo, Zuchu ameandika barua ya kuomba radhi kwa BASSFU pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa Nchini (BASATA) huku akielezea kuwa nia yake ilikuwa njema ya kutaka kutoa burudani na furaha kwa mashabiki wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here