Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Vertex Group Experts imesema inamuunga mkono juhudi za Rais Dk.samia Suluhu Hassan kwa kutangaza nchi za jirani na Afrika katikaTiba Utalii ili waweze kuwafikia wagonjwa wengi na kuongeza Pato la Taifa.
Akizungumza leo Machi 4 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Herbert Swai amesema lengo la Kampuni ni kutoa huduma za Tiba Utalii kwa kuwaunganisha wagonjwa hospitali nchini na kurahisisha urahisi wa kupata.
Amesema Kampuni hiyo tangu kuanzishwa ina muda wa miaka miwili ikiwa mikakati yao ni kuendelea kukuza Tiba utalii na kuweza zaidi ili wagonjwa wanaokuja kutibiwa na kutangaza nchi kutokana na huduma nzuri walizopata.
“Tunataka kuondoa dhana iliyojengeka kwa watu kuwa kutibiwa Hospitali ya Taifa Mhimbili ni gharama kubwa hapana tuta hakikisha wagonjwa wa nje na wandani wanapata huduma bora na kwa gharama nafuu na kwaharaka,”amesema Swai.
Amesema Rais Dk. Samia katambulisha Tanzania katika Afrika Mashariki ni kitovu cha huduma bora za afya lazima wafanyekazi ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa nje wanaokuja kutibiwa nchini.
Swai amesema Kampuni hiyo kwa takwimu za mwaka 2023 walipokea wagonjwa 47 kutoka nchi mbalimbali walitibiwa nchini katika Hospitali ya Mhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Aidha amesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya wagonjwa wanakuja kutibiwa wengine wanakuwa hawajui lugha, Kiswahili wala kingereza wanaongea lugha zao hivyo wanawakalimani kwaajili ya wagonjwa wa nje ya nchi.
Ameongeza kuwa Tiba utalii inawahusu watanzania wote na Kampuni hiyo ipo kwaajili ya kuwahudumia na kuwasiidia kupata huduma kwa haraka na ipo kisheria na inatambulika.
Akizungumza baadhi ya wagonjwa kutoka Visiwa vya Comoro waliopata huduma ya kutibiwa kupitia Kampuni hiyo, Mohamed Abdulla amesema wanaishukuru Kampuni hiyo imewawezesha kupata huduma katika Hospitali ya Taifa Mhimbili na wanaendelea vizuri.
“Tunaahaidi kuwa mabalozi wazuri na kuwashauri wananchi wa Visiwa vya Comoro kuja kutibiwa Tanzania kwasababu kuna huduma nzuri kama hauna ndugu wa kukusaidia kuna Kampuni ambayo inasimamia kuanzia matibabu yako hadi mwisho,”amesema Abdalla.