Home KITAIFA wagombea 14 wa udiwani Kimbiji warejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi...

wagombea 14 wa udiwani Kimbiji warejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo

Na Mwandishi wetu

WAGOMBEA 14 waliochukua fomu za utezi kuwania udiwani Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dares Salaam wamerejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi Mdogo wa udiwani uyakaofanyika Machi 20,2024.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kimbiji, Ricky Pascal amesema wagombea hao walianza kuchukua fomu za uteuzi kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivyopanga Februari 27 mwaka huu hadi leo Machi 4,na wote kukamilisha kujaza fomu na kuzirejesha.

“Wagombea wote waliochukua fomu za uteuzi Kata ya Kimbiji wamerejesha fomu na kutimiza matwaka ya ujazaji fomu, hivyo wagombea wote 14 wameteuliwa na tume kuwania nafasi ya Udiwani katika uchaguzi utakaofanyika Machi 20,2024,”amesema Pascal.

Pascal amewataja wagombea walioteuliwa kuwa ni Rachel Paulo Mwikola (UPDP), Halima Abdallah Mbago (NLD), Shabani Hassan Chumu ( Demokrasia Makini), Kondo Abdu Hatibu ‘Lukali’ (CUF), Diana-Rose Joseph Mhoja (ADA Tadea), Maimuna Mwinyipingu Yusufu (CCM) na Shani Ally Kitumbua (AAFP).

Wengine ni Michael Makile Mzalendo (UDP), Joyce Ephraimu Mweigule (DP), Janeth Pius Mhando (TLP),Nasra Twalib Kimo, Innocent Fratern Shirima (CCK), Neema Kassimu Yegeyege (UMD) na Juma Hassan Abdalah (NCCR-Mageuzi.

Wagombea hao walikabidhiwa fomu zao za uteuzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kimbiji, Pascal na Twidike Ntwima.

Tume ilitangaza uchaguzi Mdogo katika Kata 23 za Tanzania bara kufanyika Machi 20,2024 na fomu za uteuzi zilianza kutolewa Februari 27 hadi Machi 4 mwaka huu.

Mbali na Kata Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni), Kata zingine zinazofanya uchaguzi ni Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa (Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha), Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti), Utiri (Halmashauri ya Mji Mbinga) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).

Nyingine ni Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe), Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Mshikamano (Halmashauri ya Wilaya ya Musoma), Busegwe (Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Nkokwa (Halmashauri ya Wilaya ya Kyela), Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya Wilaya ya Meatu) Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here