Home BURUDANI HALIMA KOPWE ATINGA 10 BORA KIPENGELE CHA KAZI MRADI MISS WORLD

HALIMA KOPWE ATINGA 10 BORA KIPENGELE CHA KAZI MRADI MISS WORLD

Na Mwandishi wetu

MREMBO wa Tanzania, Halima Kopwe ameingia katika kumi bora kwenye kipengele cha ushindani cha ‘Beauty with Purpose Project’ kwenye shindano la ulimbwende la dunia (Miss World)lilowashirikisha nchi zaidi ya 100 linaloendelea nchini India

Aidha Shindano la Urembo la Dunia la 71 ambalo limeanza Februari 18, 2024 na litahitimishwa Machi 09, 2024.

Kampeni ya Halima iliyoshinda ni ‘Damu Yangu, Kizazi Changu’ ambayo ni mradi unaolenga kuboresha afya ya wanawake wajawazito na watoto nchini Tanzania na kusaidia kupunguza vya vifo vya kina mama na watoto.

Lengo kuu la kampeni yake ni kushughulikia suala la vifo vya kina mama vinavyosababishwa na kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua na upungufu wa damu kwa watoto wachanga.

Mradi huo, pamoja na mambo mengine, unajumuisha kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na kuandaa matukio ya uchangiaji damu kwa ushirikiano na kituo cha kitaifa cha Damu Salama na wadau wengine.

Zaidi ya hayo, mradi unalenga kukusanya fedha ili kusaidia vifaa vya matibabu na mahitaji mengine hospitalini kwa ajili ya uzazi salama, pamoja na kutoa bima ya afya kwa watoto wanaohitaji.

Kopwe akifanikiwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho cha mradi inaweza ikawa ndio tiketi yake ya moja kwa moja kufanikiwa kutinga 20 bora katika Mashindano hayo ya Urembo kidunia (Miss World).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here