Home KITAIFA BODI CHAMA CHA USHIRIKA CHAPAKAZI KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO MTWARA

BODI CHAMA CHA USHIRIKA CHAPAKAZI KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO MTWARA

Na Mwandishi wetu, Kibiti

MWENYEKITI wa Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoa wa Pwani, Mussa Mng’elesa ameahidi kupeleka Bodi ya Chama Cha Ushirika cha Msingi Chapakazi katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kujifunza.

Akizungumza leo Machi 4 kwenye mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika Bungu, Mwenyekiti huyo amesema vyama vya Ushirika ni uchumi hivyo vinatakiwa kuwa na wanachama wakulima na si wanasia.

“Ahadi hii kwa Chama hichi ambacho kipo Bungu Wilaya ya Kibiti imetokana na namna kinavyofanya vizuri katika kazi zake tangu kuanzishwa,”amesema Mng’elesa

Amesema Chapakazi ni kati ya vyama 10 bora kitaifa lakini pia limekuwa kikifanya vizuri kwenye suala la mapato na matumizi na kupata hati safi jambo ambalo bodi ikienda ziara za mafunzo kutakuwa na maboresho zaidi.

Mrajisi msaidizi Mkoa wa Pwani Abillahi Mutabazi amesema katika ya vyama vya Ushirika vya ufuta na korosho 98 kwa mkoa huo havizidi kumi vyenye hati inayorishisha.

Ameelekeza chama hicho kuongezea idadi ya wanachama sambamba na kuhakikisha wanajenga ghala na ofisi yao na kuachana na utaratibu wa kupanga.

Katibu wa Chapakazi Hassani Tinge amesema katika msimu wa mwaka 2023/2024 chama hicho kimepokea kipima unyevu na ubora pamoja na mashine ya kisasa ya kupulizia korosho kutoka CORECU.

Tinge amesema pia chama hicho kimefanikiwa kuongeza ubora wa korosho ambapo kg 676,543 zilizouzwa zilikuwa daraja la kwanza na kg 178,344 zilikuwa daraja la pili huku zilizo chini ya ubora zikiwa ni kg 21,971.

Amesema chama hicho kina malengo ya kujenga ofisi, ghala la kuhifadhia mazao sambamba na ukumbi wa sherehe.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here